Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:38

Siku ya Wanawake Duniani: Bado changamoto ni nyingi


Siku ya kimataifa ya wanawake imeadhimishwa Jumanne kwa kufanyika shughuli mbalimbali katika nchi tofauti huku kukitolewa mwito kwenda kwa makundi yote kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii mbalimbali.

Wanawake wa Tanzania waliadhimisha siku hiyo kwa kuzungumzia changamoto zinazo wakabili wanawake wa Kitanza katia kujikwamua kiuchumi.

Changamoto kubwa amabazo zilitajwa ni namna ya kupata mitaji kwa ajili ya kuendesha maisha yao kwa wanaotaka kujikita kwenye ujasiriamali husasan upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu.

Kwa kutambua umuhimu wa mikopo kwa wajasiriamali wanawake, katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani jijini dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu alitumia hotuba yake kuitaka benki ya wanawake kupunguza riba ya mikopo wanayotoa kwa wanawake

Waziri Ummy Mwalimu amempa siku tatu Mkurugenzi wa Benki ya wanawake Tanzania kumpatia maelezo ya sababu zinazoifanya benki hiyo kutoza riba ya asilimia kumi na tisa ya mikopo kwa wanawake huku benki nyingine zikitoza asilimia ya chini zaidi inayofikia asilimia 11.

Kwa upande wa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa upande wa mashariki mwa nchi hasa wa mkoa wa Kivu Kaskazini, mwandishi wetu Austere Malivika, aliripoti kwamba wanawake waliadhimisha siku hiyo kwa kutafakari mustakabali wao.

Mwanasheria Tudi Diam, ambaye ni mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake katika mji wa Beni, nchini DRC,amesema kwamba siku ya kimataifa ya wanawake kwa upande wake si siku ya kushererekea kwa sababu mwanamke hana hali nzuri ya maisha.

Katika ukanda huo, wanawake wameelezwa kuathiriwa hali tete ya usalama hasa mauaji yanayofanywa na vikundi vyenye silaha ikiwemo uvunjwaji wa haki za binadamu na utu wa mwanamke.

Mashirika ya wanawake nchini DRC yamekuwa yakiuomba Umoja wa Mataifa na serikali ya DRC kuwahakikishia wanawake usalama wakati wa oparesheni za kijeshi kwa sababu wao ndio wamekuwa waathirika wa kwanza.

Pamoja na tatizo la usalama, wanawake wa eneo hilo wamekuwa wakikabiliwa na huduma duni za afya hasa ya uzazi na ile ya mama na mtoto, likiwemo tatizo la watoto wadogo wa kike kutopelekwa shule.



XS
SM
MD
LG