Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:06

Wadau wa habari wasema uhuru wa vyombo vya habari bado unaminywa


Waandishi wa habari wakiwa wamejifunga tepu kwenye midomo yao wakisherehekea siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani, huko Bujumbura, Burundi , Mei 3, 2015.
Waandishi wa habari wakiwa wamejifunga tepu kwenye midomo yao wakisherehekea siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani, huko Bujumbura, Burundi , Mei 3, 2015.

Wakati waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za vyombo vya habari wanapokutana mjini Helsinki kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani hii leo, kutaonekana kutokuwepo kwa mwandishi wa habari Khadija Ismayilova ambaye hivi sasa anatumikia kifungo cha miaka 7.5 nchini Azerbaijan kutokana na kazi yake ya kuripoti kuhusu rushwa serikalini.

Kamati ya kuwalinda waandishi wa habari (CPJ), inasema waandishi wa habari wapatao 200 kama Khadija hivi sasa wapo jela duniani kote. Na jela sio njia pekee ambayo serikali inatumia kukandamiza vyombo vya habari.

Mwandishi wa habari mmoja kutoka Thailand, Pravit Rojanaphruk, pia alialikwa Helsinki lakini utawala wa kijeshi umempigia marufuku kuondoka nchini ikiwa ni matokeo ya hivi karibuni kuandika kuwa waandishi wa habari kwingineko wanakabiliwa na kifungo cha muda mrefu au hata kuuwawa.

XS
SM
MD
LG