Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 15:35

Siku ya Kimataifa ya Wanawake yaadhimishwa


Jami'an gwamnatin Najeriya suna ganawa da 'yan matan Chibok su 21 da aka sako alhamis 13 Oktoba,m 2016 a Abuja
Jami'an gwamnatin Najeriya suna ganawa da 'yan matan Chibok su 21 da aka sako alhamis 13 Oktoba,m 2016 a Abuja

Siku ya Kimataifa ya Wanawake imeadhimishwa leo Machi 8. Maelfu ya sherehe zimefanyika kote duniani kuelezea mafanikio ya wanawake katika maswala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Siku ya leo hutoa nafasi kwa wanawake kutoa mwito wa usawa ili wanawake na familia zao waweze kuishi maisha yenye ufanisi.

Margaret Kenyatta akamilisha biyo za Beyond Zero siku ya Wanawake Duniani
Margaret Kenyatta akamilisha biyo za Beyond Zero siku ya Wanawake Duniani

Mashirika mbalimbali kote duniani huchagua kauli mbiu zao kulingana na mazingira wanayoishi wanawake, wanapoadhimisha siku hii ya Kimataifa ya Wanawake.

Huko barani Afrika siku hii imeadhimishwa kwa sherehe mbali mbali.

Akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka Mombasa, mwenyekiti wa shirika la Maendeleo ya wanawake Kaunti ya Mombasa Bi. Afia Rama alisema licha ya mafanikio mengi waliopata, wanawake wengi bado wanakabiliwa na manyanyaso ya kinyumbani na ukosefu wa usawa katika sekta ya ajira.

please wait

No media source currently available

0:00 0:46:04 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Na huko Tanzania mwenyekiti wa muungano wa shirika la ‘Utepe Mweupe’ Bi. Rose Mlay aliiambia Sauti ya Amerika kuwa wanawake wengi bado wanakabiliwa na changamoto katika maswala ya uzazi salama. Alisema wengi hawana uwezo wa kupata huduma bora za afya kwao binafsi na kwa watoto wao wanapokuwa wajawazito na hata baada ya kujifungua.

Naye mke wa rais wa Kenya Bi.Margaret Kenyatta ameiadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa kutimka mbio katika uwanja wa michezo wa Nyayo Stadium kuchangia mradi wake wa ‘Beyond Zero’ unaolenga kusaidia wanawake wa Kenya kujifungua salama.

Viongozi wa vyama vya wanawake DRC
Viongozi wa vyama vya wanawake DRC

Juhudi zake zimefanikiwa kuchanga shilingi za Kenya milioni 46.

Siku ya Kimataifa ya Wanawake iliadhimishwa mwanzo mwaka wa 1911.

XS
SM
MD
LG