Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 02:30

Sierra Leonne yapitisha sheria inayolazimisha mashirika ya umma na kibinafsi kuajiri wanawake kwa % 30


Rais wa Sierra Leonne Julius Maada Bio

Sierra Leone Alhamisi imepitisha sheria inayolazimisha mashirika ya umma na kibinafsi kutenga asilimia 30 ya kazi zao kwa ajili ya wanawake, katika juhudi za kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia katika jamii inayopendelea wanaume.

Rais Julius Maada Bio alisaini mswada huo kuwa sheria, ambao pia unawahakikishia wanawake angalau wiki 14 za likizo ya uzazi, malipo sawa na fursa za mafunzo.

Bio amesema sheria hiyo “itashughulikia ipasavyo ukosefu wa usawa wa kijinsia katika nchi hii. Tunapaswa kuhakikisha kuwa inafanya kazi.”

“Lazima tukomeshe tabia ya kutoadhibu ukatili dhidi ya wanawake katika uchaguzi na maisha ya umma na kuwaadhibu watu wote na mashirika yanayopatikana na hatia ya ukatili kama huo,” aliongeza.

Wanawake nchini Sierra Leonne wanakabiliwa na ubaguzi wa kimfumo, na kulingana na shirika la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch, imekuwa ni jambo la kawaida kuwafuta kazi wanawake kama watapata ujauzito.

Wanawake wengi na wasichana wanakabiliwa pia na viwango vya juu ya ukatili wa kingono, kutokana hasa na tabia ya kutumia ubakaji kama silaha wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka wa 1991 hadi 2002.

Sheria hiyo mpya inalenga pia kuboresha mfumo wa kutoa mikopo kwa wanawake katika nchi ambapo wamekuwa hawapati kabisa mikopo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG