Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:33

Siasa za kupata katiba mpyaTanzania zapamba moto


Wabunge wakiwa ndani ya bunge maalumu la katiba mjini Dodoma, Tanzania
Wabunge wakiwa ndani ya bunge maalumu la katiba mjini Dodoma, Tanzania
Uteuzi wa wajumbe watano watakaoingia kwenye kamati ya uongozi uliofanywa na Mwenyekiti wa bunge maalum la katiba, Bw. Samwel Sitta umeleta mvutano mkubwa miongoni mwa wajumbe baada ya kuutangaza.

Hata hivyo uteuzi huo utakaoambatana na wenyeviti wengine waliochaguliwa kwenye kamati 12 ulichukuliwa na baadhi ya wajumbe kwa hisia tofauti za kutoaminiana kwa kazi wanayokwenda kuifanya mbele yao ya kuandika katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mjumbe mwingine John Mnyika alisema kamati hiyo itaendelea kulalamikiwa sio tu kwa kukosa uwiano wa pande mbili za muungano bali hata katika upande mmoja wa muungano kukosa sura kabisa ya uwakilishi jambo ambalo alisema halieleweki.

Hata hivyo Profesa Lipumba wa chama cha CUF alikanusha kuwa yeye ni mwenyekiti wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA na kusema kuwa mwenyekiti wake ni Bw. Freeman Mbowe wa chama cha CHADEMA. Lipumba alisema katika hali inavyokwenda katika bunge hilo ni wazi kabisa kwamba hakuna nia njema ya kupata katiba ya wananchi.

Aidha wajumbe wengine walipinga uteuzi huo ambao una wawakilishi kutoka chama tawala cha CCM na kumshauri mwenyekiti huyo wa bunge kufikiria upya juu ya uteuzi alioufanya bila kuegemea vyama vya kisiasa.

Kwa upande mwingine mmoja wa wajumbe aliyesimama kwa muda mrefu kuomba muongozo wa mwenyekiti bila ya mafanikio Bw. Ezekiel Oluochi amedai kuwa randama ya pili ya rasimu ya katiba, ambayo ndiyo yenye uchambuzi wa kina wa mambo yanayobishaniwa hawana wajumbe wengi wa bunge hilo maalum la katiba.
XS
SM
MD
LG