Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:40

Katumbi akutana na waendesha mashtaka mjini Lubumbashi


Moise Katumbi akiwasili mahakamani.
Moise Katumbi akiwasili mahakamani.

Kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Moise Katumbi, anatarajiwa kufikishwa mbele ya kiongozi wa mashtaka hii leo kujibu maswali kuhusu shutuma kwamba aliwaajiri mamluki wa kutoka nchi za nje.

Hayo ni kwa mujibu wa wakili wa mwanasiasa huyo. Serikali ya Joseph Kabila imesema iko na ushahidi wa nyaraka unaoonyesha kwamba waliokuwa wanajeshi wa Marekani, wanamfanyia kazi Katumbi kama walinzi wake katika mkoa wa Katanga.

Lakini Katumbi, ambaye ni mfanyabiashara tajiri na kiongozi wa klabu maarufu cha kandanda, T-P MAZEMBE, amekanusha madai hayo. Wiki jana, Katumbi alikubali shinikizo la muungano wa vyama saba vya upinzani, kumtaka awe mpinzani wa Joseph Kabila kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Serikali ilitoa shutuma hizo, dhidi yake, siku hiyo hiyo alipokubali shinikizo hilo kutoka kwa muungano wa vyama vya kisiasa.

XS
SM
MD
LG