Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 08:40

Shuhuda wa mauaji ya Nemtsov hakumuona muuaji


Rafiki wa kike wa kiongozi wa upinzani aliyeuwawa Boris Nemtsov, ambaye alikuwa naye wakati anashambuliwa karibu na ikulu ya Kremlin mwishoni mwa juma lililopita anasema hakumuona muuaji.

Nemtsov alikuwa anavuka daraja na Anna Duritskaya, mwanamitindo wa Ki-Ukraine, mwenye miaka 23 ambaye wachunguzi wanasema alipigwa risasi mara nne mgongoni na mtu aliyekuwa kwenye gari lililokuwa linapita.

Katika maelezo yake ya kwanza hadharani tokea mauaji hayo, Duritskaya, amesema katika mahojiano na televisheni binafsi ya Russia, kwamba yeye na kiongozi huyo walikuwa wanavuka daraja kuelekea katika makazi yake muda mfupi kabla ya saa sita usiku.

Anasema muuaji aliwafikia kutoka nyuma na gari na baada kufanya mauaji gari hilo liliondoka eneo la tukio.

Lakini Duritskaya, anasema hakumona aliyeshambulia wala kukumbuka aina ya gari wala nambari zake za liseni.

XS
SM
MD
LG