Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:54

Waliokufa katika tetemeko la Taiwan wafikia 9


Timu za waokoaji zikijaribu kutafuta manusura wa tetemeko la ardhi nchini Taiwan.
Timu za waokoaji zikijaribu kutafuta manusura wa tetemeko la ardhi nchini Taiwan.

Timu za waokoaji katika eneo la mashariki mwa nchi ya Taiwan zimeendelea Alhamisi kuchimba vifusi vya jengo la makazi lililoporomoka baada ya tetemeko la ardhi la Jumanne.

Maafisa wa idara ya zima moto kwenye kisiwa hicho wamesema kuwa idadi ya vifo hadi sasa imefikia watu 9 na sio 10 kama iliovyotangazwa hapo awali.

Pia wamefafanua kuwa idadi ya watu wasiojulikana mahali walipo imeshuka kutoka 60 hadi 10.

Takriban watu watatu miongoni mwa waliokufa ni kutoka China. Jengo hilo la ghorofa 12 na ambalo ni maarufu kwa watalii liliharibiwa vibaya na tetemeko hilo lenye nguvu ya 6.4 katika kipimo cha rikta.

Zaidi ya watu 250 walijeruhiwa kwenye tukio hilo ambalo pia liliacha majengo mengine matatu ya ghorofa yakiwa yameinama ikiweko hoteli ya Marshal ambapo watu wawili walikufa.

Zaidi ya watu 800 walikesha kwenye mehema wengi wao wakiogopa kurudi nyumbani kwa kuhofia kurudi tena kwa tetemeko hilo.

Tanzania

XS
SM
MD
LG