Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 17:36

Shirika la ndege la Kenya latarajia kupata faida mwaka huu


Ndege ya shirika la ndege ya Kenya
Ndege ya shirika la ndege ya Kenya

Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Kenya Allan Kilavuka amesema Jumanne kwamba shirika hilo linalenga kuongeza mapato yake kwa asilimia 20 mwaka huu.

Ameongeza kusema pia kwamba shirika lake linajitahidi kuongeza wasafiri ili kujikwamua kutokana na athari za janga la corona. Kilavika amesema kwamba baada ya miaka miwili ya kipindi kigumu kutokana na janga hilo , wanatarajia ongezeko la wasafiri mwaka huu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ongezeko hilo litategemea kutokuwepo kufungwa kwa shughuli za kawaida kutokana na virusi vya Covid. Amesema pia kwamba anatumai uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti hautaathiri kipindi cha watalii kama ilivyo shuhudiwa katika miaka ya nyuma.

Shirika la ndege la Kenya ambalo pia linajulikana kama KQ linamilikiwa kwa asilimia 48.9 na serikali, na lilishuhudia kushuka kwa nusu ya mapato yake wakati wa janga la corona katika miaka miwili iliyopita. Mapato kutokana na wasafiri yaliongezeka kwa asilimia 21 mwaka jana, na kusaidia shirika hilo kupunguza hasara yake kwa theluthi 5 katika nusu ya kwanza ya mwaka jana. Licha ya hilo, hasara ya shilingi bilioni 11.5 bado ilipatikana katika kipindi hicho.

XS
SM
MD
LG