Shirika hilo ambalo ni moja ya mashirika makubwa sana ndege barani Afrika, limesema kwamba uhaba huo ambao unashuhudiwa kote ulimwenguni utaathiri safari zake kwa takriban wiki mbili.
Taarifa ambayo Reuters imeiona leo Jumatatu imesema kwamba, “Changamoto zilizopo zitaongeza muda wa ukarabati wa ndege zetu, wakati pia zikipelekea kusitishwa kabisa kwa safari za ndege moja au mbili.”
Mara ya kwanza Kenya Airways kulalamikia uhaba wa vipuri ilikuwa Januari mwaka huu, wakati huo ikelezea kuwa uhaba huo umetokana na vita vya Ukraine ambavyo vilizuia mfumo wa usambazaji wa Russia kwa sekta ya anga ulimwenguni.
Forum