Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:03

Shirika la ndege la Ethiopia limeingia makubaliano ya safari na Airlink ya Afrika kusini


Mojawapo ya ndege za shirika la ndege la Ethiopia
Mojawapo ya ndege za shirika la ndege la Ethiopia

Makubaliano ya hivi karibuni yanawawezesha wasafiri kununua tiketi moja ya kusafiri kupitia njia yeyote kati ya ndege hizo ikiunganisha miji midogo ya Afrika kusini na kufika anga ya kimataifa ya Ethiopia

Shirika la ndege la Ethiopia limeingia makubaliano ya kushirikiana njia za safari na shirika la ndege la Airlink, la Afrika kusini, wakati shirika hilo kubwa zaidi la ndege barani Afrika, linapanua njia ya safari zake.

Shirika la ndege la Ethiopia, limeingia katika mfululizo wa ushirikiano na mashirika ya ndege katika bara hilo na ulimwengu. Makubaliano ya hivi karibuni yanawawezesha wasafiri kununua tiketi moja ya kusafiri kupitia njia yeyote kati ya ndege hizo ikiunganisha miji midogo ya Afrika kusini na kufika anga ya kimataifa ya Ethiopia.

Airlink yenye makao yake Johannesburg ni huduma kuu ya anga ya Afrika kusini kati ya miji midogo na mikubwa. Shirika la ndege la kitaifa la Afrika kusini (SAA), hivi karibuni liliibuka kutoka kwa uokoaji wa biashara wa miezi 17, na kuanza tena huduma chache za safari za ndani na kikanda mwezi uliopita.

XS
SM
MD
LG