Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:47

Shirika la Msalaba Mwekundu laonya kuhusu vita vya Ukraine


Mashambulizi ya Russia mjini Mariupol, Ukraine kwenye picha ya awali
Mashambulizi ya Russia mjini Mariupol, Ukraine kwenye picha ya awali

Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na jamii ya Mwezi Mwekundu wameonya juu ya vita virefu nchini Ukraine, kwamba huenda vitasababisha madhara makubwa sana ya kibinadamu na kuwa mzozo mwingine wa ulimwengu.


Athari kuu kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine tayari zimeonekana miezi sita baada ya uvamizi huo . Maafisa wa shirikisho la kimataifa la msalaba mwekundu wameonya kwamba athari za kiuchumi kwa mamilioni ya watu wenye shida kote duniani zitazidi kuwa mbaya zaidi kadri vita vinayoendelea kwa muda mrefu. Ukraine ni moja ya muuzaji mkubwa sana duniani wa nafaka kabla ya vita kuanza.

​Vizuizi vya Russia kwenye bandari ya Black Sea hata hivyo vimezuia usafirishaji wa shehena za nafaka, na kuchochea mzozo mkubwa wa chakula duniani. Kupanda sana kwa bei za vyakula na mafuta kumesababisha bidhaa hizo muhimu kushindwa kununuliwa, na kuwatumbukiza mamilioni ya watu katika hatari ya njaa.

XS
SM
MD
LG