Shirika la Mpango wa Chakula Duniani lilisema Ijumaa kwamba hatimaye limeweza kupeleka msaada wa chakula unaohitajika sana katika eneo lililokumbwa na vita la Darfur kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadha huku likionya kwamba vita vya Sudan vinaweza kusababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani.
Shirika hilo la chakula la Umoja wa Mataifa lilisema misafara miwili ilivuka mpaka kutoka Chad hadi Darfur mwishoni mwa juma lililopita, ikibeba msaada wa chakula na lishe kwa takriban watu robo milioni kaskazini, magharibi na katikati mwa Darfur.
Ilisema ujumbe huo uliocheleweshwa kwa muda mrefu ulipewa idhini ya kuendelea kufuatia mazungumzo marefu ya kufungua tena njia za msafara baada ya vikosi vya Wanajeshi wa Sudan kufuta kibali cha njia za kibinadamu kutoka Chad mwezi Februari.
Operesheni za kuvuka mpaka kutoka Chad hadi Darfur ni muhimu kufikia jamii ambapo watoto tayari wanakufa kwa utapiamlo, alisema Leni Kinzli, afisa wa mawasiliano wa WFP wa Sudan.
Forum