Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:21

Shirika kongwe la haki za binadamu lafutwa Burundi


Warundi wanaoishi nje ya Burundi wakimtaka Rais Pierre Nkurunziza kuachia madaraka.
Warundi wanaoishi nje ya Burundi wakimtaka Rais Pierre Nkurunziza kuachia madaraka.

Mkuu wa shirika hilo la iteka, Ancher Nikoyagize ameondoka nchini Burundi kwa kuhofia usalama wake.

Shirika la kutetea haki za binadamu la ITEKA nchini Burundi limepigwa marufuku.

Mwandishi wetu Haidallah Hakizimana amesema shirika hilo ambalo ni kongwe kuliko yote nchini humo linatuhumiwa kwenda kinyume na majukumu yake na kushirikiana na maadui.

Amesema hatua hii imechukuliwa baada ya shirika hilo kuchapisha ripoti inayotuhumu serikali ya Burundi kuhusika na matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu kufuatia mzozo wa kisiasa unaoikabili Burundi tangu April 2015.

Hili limekuwa shirika la sita kufutwa nchini humo kati ya mashirika yaliyokuwa mstari wa mbele kupinga rais Pierre Nkurunziza asigombee muhula wa tat

Shirika hilo linalotetea haki za binadamu la ITEKA lina zaidi ya miaka 25 katika kupigania haki za binadamu nchini Burundi.

Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Ndani mwenye mamlaka ya kufuatilia shughuli za mashirika ya kiraia amesema hatua ya kufuta usajili wa shirika hilo umetokana na shirika hilo kwenda kinyume na majukumu yake na kushirikiana na maadui wa demokrasia.

Kwa mujibu wa msaidizi wa waziri huyo, Therence Ntahiraja amesema siku za nyuma shirika la Iteka, licha ya kuwa lilisimamishwa kwa muda kwa sababu ya ripoti iliyokuwa imejaa uongo.

Aliongeza kusema kutokana na hayo wizara iliamuru kuangalia upya usajili wa shirika hilo na hivyo kulifuta mara moja.

Ripoti iliyotajwa hapo juu, ilichapishwa kwa ushirikiano na shirika la kutetea haki za binadamu la IFDH lenye makao yake Paris, Ufaransa.

Kulingana na ripoti hiyo serikali na makundi mengine yalinyooshewa vidole kwamba yalihusika na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.

Mkuu wa shirika hilo, Ancher Nikoyagize aliondoka nchini Burundi kwa kuhofia usalama wake.

Mweka hazina wa shirika hilo, Bi. Claudette Kwizera alitekwa nyara mjini Bujumbura mwishoni mwa mwaka 2015 na hadi sasa hatima yake haijulikani.

Mashirika mengine matano ya kutetea haki za binadamu ambayo yalikuwa mstari wa mbele kupinga rais wa Burundi Nkurunziza kugombea awamu ya watu mwaka jana yalipigwa marufuku.

XS
SM
MD
LG