Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 18:11

Shinikizo laongezeka kwa Rais Putin kutolewa katika mkutano wa G20


Rais Vladimir Putin

Rais Joe Biden, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison, kati ya viongozi wengine, ambao wameeleza wasiwasi wao juu ya ushiriki wa Putin katika mkutano huo na kuashiria hawatahudhuria iwapo Putin atakuwepo.

White House inaashiria kuwa uamuzi wa Indonesia – inayoshikilia mwaka huu nafasi ya urais wa nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani, G20 – kuikaribisha Ukraine katika mkutano wa viongozi wa Novemba huko Bali haitoshi kuhakikisha uwepo wa Rais wa Marekani Joe Biden – mpaka pale Rais wa Russia Vladimir Putin atakapotolewa katika mkusanyiko huo.

“Tunavyo fahamu, na pia nyinyi mnaweza kulithibitisha hili na Waindonesia, kwani tumewasiliana nao kwa faragha, ni kwamba walikuwa wameikaribisha[Russia] kabla ya uvamizi huo. … Tumepeleka maoni yetu kwamba hatufikirii wao [Russia] wanatakiwa kuhudhuria, " msemaji wa White House Jen Psaki aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa.

Mapema Ijumaa, Rais wa Indonesia Joko Widodo alitangaza kuwa alikuwa amemwualika Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kuhudhuria mkutano wa huo wa uchumi.

“Tunafahamu kuwa G-20 ina jukumu katika kufufua uchumi wa dunia, na tunapozungumzia kufufua uchumi wa dunia, hivi sasa kuna vigezo viwili muhimu: COVID-19 na vita nchini Ukraine,” Widodo alisema katika maoni yake kwa njia ya video, akionyesha busara yake katika kumualika Zelenskyy.

Widodo alisema alikuwa amemwalika Zelenskyy wakati wa mazungumzo ya simu naye siku ya Jumatano, wakati ambapo Widodo alikataa ombi lake la silaha lakini alitoa misaada ya kibinadamu kwa Ukraine. Alisema kuwa alikuwa ameongea na Putin Alhamisi na kuwa Rais wa Russia alimweleza kuwa atahudhuria mkutano huo.

“Indonesia inataka kuziunganisha nchi wanachama wa G-20,” Widodo alisema. “Amani na utulivu ni muhimu kwa ajili ya kufufua na kukuza uchumi.”

Huenda hilo likaonekana pengine si rahisi wakati viongozi wa Magharibi wanataka Russia iondolewe katika kundi hilo la nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani.

Biden, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison, kati ya viongozi wengine, ambao wameeleza wasiwasi wao juu ya ushiriki wa Putin katika mkutano huo na kuashiria hawatahudhuria iwapo Putin atakuwepo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG