Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 18:15

Shinikizo dhidi ya Gbagbo laendelea


Rais aliyeng'ang'ania madaraka Ivory Coast Laurent Bgagbo
Rais aliyeng'ang'ania madaraka Ivory Coast Laurent Bgagbo

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe amesema Jumanne kuwa wasuluhishi wapo karibu kabisa kumridhisha Bw. Gbagbo kuachia madaraka.

Rais aliyepo madarakani Ivory Coast Laurent Gbagbo anazungumzia namna ya kujisalimisha baada ya majeshi ya mpinzani wake kuzingira nyumba yake Jumanne.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe alisema Jumanne kuwa wasuluhishi wapo karibu kabisa kumridhisha Bw. Gbagbo kuachia madaraka.

Baadaye alisema Ufaransa na Umoja wa mataifa unataka Bw. Gbagbo asaini nyaraka ambayo ya kukubali kuachia madaraka na kumtambua Alassane Ouattara kama rais.

Wakati huo, huo Rais wa Marekani Barack Obama amesema kiongozi huyo mkaidi wa Ivory Coast lazima aachie madaraka mara moja ili kuzuia umwagaji damu na kumaliza ghasia ambazo zimegubika nchi hiyo.

Bw. Obama alisema katika taarifa yake Jumanne kwamba anaunga mkono kwa hali ya juu hatua ya walinda amani na majeshi ya Ufaransa, walioshambulia ngome ya Gbagbo jumatatu kwa lengo la kulinda raia.

XS
SM
MD
LG