Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:18

Shida ya vipuri yaathiri safari za Kenya Airways


Safari ya kwanza ya shirika la ndege la Kenya Airways kuelekea Marekani katika uwanja wa ndege wa JFK mjini New York.
Safari ya kwanza ya shirika la ndege la Kenya Airways kuelekea Marekani katika uwanja wa ndege wa JFK mjini New York.

Shirika la ndege la Kenya Airways linakumbana na changamoto za kutibua  safari zake kutokana na uchelewesho wa  kupata vipuri vya ndege vinavyohitajika kwa matengenezo, shirika hilo  lilisema Jumatatu jioni.

Shirika hilo ambalo ni mojawapo ya makampuni makubwa zaidi barani Afrika, huenda likalazimika kupunguza baadhi ya safari za ndege iwapo changamoto za kupata vifaa hivyo zitaendelea, Afisa Mtendaji Mkuu Allan Kilavuka alisema katika taarifa yake.

Changamoto zimesababishwa na mzozo wa vita vya Ukraine, ambao umelemaza kwa kiasi kikubwa mlolongo wa usambazaji wa Russia muhimu kwa usafiri wa anga duniani," alisema.

Aliitaja Titanium kutoka Russia kuwa ni moja ya malighafi muhimu inayotumiwa na sekta ya anga, na ni muhimu kwa matengenezo ya ndege.

XS
SM
MD
LG