Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 00:57

Sheria mpya ya uhamiaji yaanza Arizona


Sheria mpya ya uhamiaji imeanza kufanya kazi katika jimbo la Arizona nchini Marekani lakini bila vipengele vilivyozusha ubishani.

Sheria mpya ya uhamiaji imeanza kufanya kazi katika jimbo la kusini-magharibi mwa Marekani - Arizona - lakini bila ya baadhi ya vipengele vilivyozusha mabishano makubwa.

Jaji mmoja wa Marekani alitoa amri ya muda kusimamisha baadhi ya vipengele hivyo Jumatano hasa kuhusu kipengele kinachoruhusu polisi kumtaka mtu atoe hati zake za uhamiaji wanapomsimamisha kwa kosa lolote lile, hasa wakishuku kwamba yuko nchini kinyume cha sheria.

Jaji huyo pia amesimamisha kwa muda kipengele kinachotaka wahamiaji kuwa wanabeba hati zao za uhamiaji wakati wote, na sheria ambayo inazuia wahamiaji walio nchini kinyume cha sheria kuomba kazi katika maeneo ya umma.

Hata hivyo, Gavana wa jimbo la Arizona Jan Brewer anasema "mapambano bado hayajamalizika." Katika taarifa aliyotoa Jumatano, Brewer alisema yuko tayari "kupambana mpaka mahakama kuu."

XS
SM
MD
LG