Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:54

Sheria mpya Israel yapendekezwa kupunguza nguvu ya mahakama


Waziri wa Sheria wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumatano alizindua  pendekezo la muda mrefu la serikali mpya la kufanyia marekebisho mfumo wa mahakama.

Marekebisho hayo yanalenga kuidhoofisha Mahakama ya Juu ya nchi hiyo.

Wakosoaji waliishutumu serikali kwa kutangaza vita dhidi ya mfumo wa sheria, wakisema mpango huo utavuruga mfumo wa ukaguzi na mizani wa Israel na kudhoofisha taasisi zake za kidemokrasia.

Vilevile imeelezwa mpango guo utatoa nguvu kamili katika muungano wa mrengo mkali wa kulia katika historia ya nchi hiyo.

Waziri wa Sheria Yariv Levin, msiri wa Netanyahu na mkosoaji wa muda mrefu wa Mahakama ya Juu, aliwasilisha mpango wake siku moja kabla ya majaji kujadili sheria mpya.

Sheria hiyo yenye utata iliyopitishwa na serikali inamruhusu mwanasiasa aliyepatikana na hatia ya makosa ya kodi kuhudumu kama waziri.

XS
SM
MD
LG