Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 22:26

Sheinbaum ameshinda urais Mexico


Mgombea wa urais kwa chama kinachotawala nchini Mexico Claudia Sheinbaum akihutubia wafuasi wake baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza mshindi June 3, 2024
Mgombea wa urais kwa chama kinachotawala nchini Mexico Claudia Sheinbaum akihutubia wafuasi wake baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza mshindi June 3, 2024

Mshindi wa tuzo ya Nobel ya sayansi ya mazingira Claudia Sheinbaum, ameshinda kura za urais nchini Mexico na kuwa mwanamke wa kwanza katika wadhifa huo.

Sheinbaum,mwenye umri wa miaka 61, amepata ushindi mkubwa na kuahidi kuendelea kufanya kazi ya mtangulizi wake, Andres Manuel Lopeza Obrador anayeondoka madarakani.

Kulingana na taasisi ya kitaifa ya uchaguzi INE, Sheinbaum, amepata kati ya asilimia 58.3 na 60.7 ya kura zilizopigwa.

Ushindi huo ndio mkubwa zaidi kuwahi kurekodiwa na mgombea wa urais katika uchaguzi wa Mexico tangu kumalizika kwa siasa za chama kimoja, mwaka 2000.

Akitoa hotuba ya kukubali ushindi, Sheinbaum amemshukuru Lopez Obrador akimtaja kuwa kiongozi wa kipekee aliyeibadilisha Mexico kimaendeleo.

Obrador aliongeza kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi mara mbili, kupunguza kiwango cha umaskini, kuimarika kwa sarafu ya Mexico – peso, na kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira.

Forum

XS
SM
MD
LG