Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:57

Wajitoa mhanga wawili walipua kituo cha kijeshi Yemen


Aden, nchini Yemen
Aden, nchini Yemen

Jeshi la Yemen limesema kuwa watu wawili wa kujitoa muhanga wameshambulia kituo cha kijeshi kilicho karibu na uwanja wa ndege wa Aden nchini Yemen kwa kutumia mabomu ya kwenye gari mapema leo Jumatano.

Takriban watu sita wameuwawa huku maafisa wa usalama wakisema kuwa mashambulizi ya bunduki yalifuata muda mfupi baada ya mabomu kuteguliwa.

Shambulizi hilo limetokea wakati wa siku kuu ya Kiislamu ya Eid al-Fitr inayoashiria kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Mji wa Aden umekuwa makao makuu ya muda ya Serikali inayoungwa mkono na Saudi Arabia lakini mashambulizi yameendelea kushuhudiwa mara kwa mara.

Washambuliaji wa kujitoa muhanga kutoka kundi la Islamic State walishambulia na kuuwa wanafunzi wa kijeshi 45 kwenye kituo kimoja cha kijeshi mjini Aden mwezi Mei.

XS
SM
MD
LG