Mlipuko umeua watu 26 na kujeruhi wengine 60.
Afisa wa ngazi ya juu wa polisi Mohammad Baloch amewaambia waandishi wa habari kwamba mlipuko mkubwa katika mji mkuu wa Quetta ulitokea katika sehemu ya abiria kusubiri treni na kwamba sehemu hiyo ilikuwa na karibu watu 100 wakati wa tukio.
Karibu nusu ya waliofariki na wengi wa waliojeruhiwa ni wanajeshi wa Pakistan, ambao inaaminika ndio waliokuwa wamelengwa katika shambulizi hilo.
Msemaji wa serikali ya jimbo Shahid Rind, amesema kwamba watu 10 kati ya waliojeruhiwa wapo katika hali mahututi.
Kundi la wapiganaji la Baloch, limedai kuhusika na shambulizi hilo.
Forum