Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 13:38

Shambulizi la Ukraine, lasababisha maafa Russia


Shambulizi la ndege zisizo na rubani za Ukraine, la Jumatano kwenye ghala la Russia, limesababisha mlipuko kama wa tetemeko la ardhi na kuwasha moto ambao ulilazimisha kuhamishwa kwa mji katika mkoa wa Tver nchini Russia.

“Adui alishambulia ghala la risasi katika eneo la Toropets,” amesema Yuri Podolyaka, mzaliwa wa Ukraine, mwanablogu wa kijeshi anayeunga mkono Russia, shirika la habari la Reuters limeripoti.

Wachunguzi wa tetemeko la ardhi walichukulia tukio hilo kama tetemeko la ardhi, na satelaiti za NASA zilibainisha chanzo kikubwa cha joto katika eneo hilo hilo. Igor Rudenya, gavana wa eneo la Tver, amesema kwenye mtandao wa Telegram kwamba ndege zisizo na rubani zilitunguliwa na moto uliwaka, lakini hali hiyo ilidhibitiwa.

Reuters imeonyesha kile ilichosema video ambayo haijathibitishwa ya mlipuko wa ghala kwa taasisi ya George William Herbert.

Forum

XS
SM
MD
LG