Idadi ya waliofariki dunia inaongezeka katika jiji la pili kwa ukubwa nchini humo wakati lilikumbwa na mashambulizi mawili siku moja iliyopita.
Mabomu mawili yaliyolenga hapo yaliharibu duka la DIY katika eneo la makazi ya jijini humo Jumamosi mchana, Gavana wa mkoa Oleh Syniehubov, alisema kwenye televisheni ya taifa.
Mashambulizi hayo yalisababisha moto mkubwa ambao na moshi mzito mweusi ulisambaa mamia ya mita angani.
Watu 43 walijeruhiwa ofisi ya waendesha mashtaka wa eneo imesema. Meya wa Kharkiv, Ihor Terekhov amesema takriban watu 120 walikuwepo katika duka la vifaa wakati mabomu yalipolipuka.
Forum