Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 10, 2025 Local time: 23:36

Shambulizi la Russia katika eneo la mashariki mwa Ukraine  laua mtu mmoja


 Matokeo ya shambulio la kombora la Russia huko Kherson.
Matokeo ya shambulio la kombora la Russia huko Kherson.

Gavana wa Kherson Oleksandr Prokudin alisema shambulizi la Russia katika eneo la mashariki mwa Ukraine  liliua mtu mmoja, kujeruhi wengine wawili na kuharibu majengo katikati mwa jiji siku ya Jumatano

Tukio la kutisha tena Prokudin alisema katika ujumbe kwenye programu ya Telegram. Vioo vilivyovunjika, madirisha yaliovunjwa nyumba zilizoharibiwa. Watu wenye sauti za kutetemeka walisimulia kile ambacho wamepitia.

Mapema Jumatano, waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine aliripoti kwamba Russia ilishambulia kwa makombora makazi 118 katika mikoa 10, zaidi ya katika kipindi kingine chochote cha saa 24 katika mwaka uliopita.

Shambulio la ndege zisizo na rubani la Russia limeripotiwa kumuua raia mwingine huko Nikopol, kwenye ukingo wa pili wa Mto Dniper kutoka kwenye kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia kinachoshikiliwa na Russia.

Watu wengine wanne walijeruhiwa katika shambulio hilo, Gavana wa eneo Serhii Lysak alisema

Forum

XS
SM
MD
LG