Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 14:36

Watu 10 wauwawa kwa bomu Cameroon


Djakana, Cameroon

Takriban watu 10 wameuwawa kwenye shambulizi la kigaidi kaskazini mwa Cameroon Jumatano jioni.

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga kutoka kundi la Boko Haram alitegua vilipuzi alivyokuwa amejifungilia nje ya msikiti karibu na mpaka wa Nigeria. Shambulizi hilo lilitokea wakati wa kufungua mfungo wa siku katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Wengi walioathiriwa ni kutoka kundi linalopigana na wanamgambo wa Boko Haram kutoka eneo hilo. Maafisa wa polisi wamesema kuwa mshambuliaji alikuwa mvulana mdogo.

Kundi la Boko Haram limekuwa likifanya mashambulizi nchini Cameroon wakati mwingine likitumia wasichana wadogo kuuwa darzeni ya watu wakiwa kama washambuliaji wa kujitoa muhanga. Kundi hilo lenye makao yake Nigeria limekuwa likifanya mashambulizi kwenye nchi jirani za Chad, Niger na Cameroon kwa miaka 7 sasa ikiwa juhudi ya kuunda kalifa ya kiislamu.

XS
SM
MD
LG