Haijafahamika wazi ikiwa kamanda Mohammed Deif ni miongoni mwa watu walouwawa.
Maafisa wa Israel wamethibitisha kwamba yeye pamoja na kamanda mwengine wa Hamas Rafa Szlama ndio walikua wanalengwa.
Jeshi la Israel limesema kwamba linachunguza na kuhakikisha kuhusu matokeo ya shambulio hilo.
Deif anaaminika kuwa ndiye mtayarishaji mkuu wa sahmbulio la Oktoba 7b lililosababisha vifo vya watu 1 200 kusini mwa Israel na kuzusha vita kati ya Israel na Hamas.
Yeye ni kamanda wa pili chini ya Yahya Sinwar mkatika Hamas ni jina lake liko juu kwenye orodha ya watu wanaotafuta na Israel kwa miaka mingi na inaaminika amenusurika majaribio kadhaa ya kuuliwa na Israel.
Ikiwa Deif ameuliwa mazungumzo ya usitishaji mapigano yanaweza kuvurugika kutokana na kile kitakacho chukuliwa ni ushindi mkubwa kwa Israel katika vita hivyo vya miezi 9
Forum