Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:57

Shambulizi la gruneti lauwa Nairobi


Kanisa lililoshambuliwa Nairobi kwa gruneti, Aprili 29, 2012
Kanisa lililoshambuliwa Nairobi kwa gruneti, Aprili 29, 2012

Mtu mmoja auawa na wengine zaidi ya 10 wajeruhiwa kanisani Nairobi

Polisi nchini Kenya wanasema shambulizi la gruneti kwenye Kanisa moja jijini Nairobi limeuwa mtu mmoja Jumapili na kuwajeruhi vibaya wengine zaidi ya 10. Mpaka sasa hakuna aliyedai kufanya shambulizi hilo katika Kanisa hilo linalojulikana kama God’s House of Miracle International church lililoko katika mji mkuu wa Kenya.

Polisi bado wanachunguza tukio hilo. Shambulizi la Jumapili limefanyika siku 6 baada ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya kuonya juu ya uwezekano wa shambulizi la kigaidi mjini Nairobi. Ubalozi huo ulitoa ujumbe huo ukionya raia wa Marekani kutahadhari.

Ubalozi huo ulisema una habari za kuaminika kuwa huenda mahoteli na majengo mashuhuri ya serikali mjini Nairobi yakashambuliwa na magaidi. Aidha taarifa hiyo ya ubalozi ilisema wakati mahsusi wa shambulizi hilo hujulikani lakini yaaminika wanaopanga shambulizi hilo wamo katika hatua za mwisho.

XS
SM
MD
LG