Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 22:27

Watu 20 wauwawa Somalia katika mlipuko


Mogadishu na Afgoye, Somalia
Mogadishu na Afgoye, Somalia

Maafisa wa Somalia wamesema takriban watu 20 wameuwawa kwenye shambulizi la bomu kando ya barabara lilololenga basi la abiria kwenye njia kuu inayounganisha Mogadishu na Afgoye kilomita 30 magharibi mwa mji mkuu.

Afisaa wa Polisi kwenye eneo la tukio, Abdikadir Mohamed, ameambia shirika la habari la Reuters kuwa bomu hilo liliteguliwa na mtu aliekuwa mbali.

Naibu Mwenyekiti wa mji wa Afgoye, Abdullahi Hassan, ametembelea eneo na kuambia VOA kuwa basi hilo limeharibiwa kabisa wakati wa shambulizi hilo lililofanyika mapema leo.

Hakuna yeyote aliedai kuhusika ingawa kundi la wanamgambo la Al-Shaabab limekuwa likifanya mashambulizi sawa na hayo dhidi ya Serikali pamoja na walinda ambao ni kutoka kikosi cha Umoja wa Afrika.

XS
SM
MD
LG