Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 20:03

Shambulizi la Bomu Nigeria lauwa watu sita


Mhanga wa kujitolea auwa watu sita Maiduguri

Mamlaka za Nigeria zinasema takriban watu sita wameuawa katika shambulizi la bomu lililofanywa na mhanga wa kujitolea katika mji wa Maiduguri. Polisi wanasema mshambuliaji huyo alilipua gari lake nje ya makao makuu ya mji huo Ijumaa. Askari polisi ni miongoni mwa waliouawa na takriban watu saba kujeruhiwa. Shambulizi hilo lilifanywa siku moja baada ya ubalozi wa Marekani nchini Nigeria kuwashauri raia wake kuondoka mji wa Maiduguri kutokana na ghasia zinazoendelea mjini humo. Siku ya Alhamis ubalozi huo ulionya juu ya ghasia baina ya makundi ya watu wenye siasa kali na vikosi vya serikali. Aidha ubalozi huo ulisema unaamini hali katika mji wa Maiduguri itaendelea kuwa tete. Hakuna kundi lililodai kuwajibika kwa shambulizi la Ijumaa . Lakini katika siku za nyuma kundi la wanamgambo wa kiislam Boko Haram limekiri kufanya mashambulizi kama hayo. Maiduguri ni ngome kuu ya kundi la Boko Haram, kundi linalolaumiwa kwa mauaji ya mamia ya raia wa Nigeria. Kundi hilo limesema litaka kuunda taifa la Kiislam Kaskazini mwa Nigeria na kwamba halitambui serikali ya Nigeria wala katiba yake. Taifa hilo lenye watu milioni 150 ligawanyika nusu kwa nusu lkati ya Waislam wanaoishi kaskazini na Wakristo wanaoishi kusini mwa nchi.

XS
SM
MD
LG