Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 01:52

Shambulizi la bomu laua zaidi ya 17 msikitini Afghanistan


Mwanamme aliyejeruhiwa katika shambulizi la bomu katika msikiti wa washia akipokea matibabu hospitalini April 21, 2022. PICHA: AFP

Shambulizi la bomu katika msikiti wa washia, uliokuwa umejaa waumini, limeua watu 17 na kujeruhi wengine 52 nchini Afghanistan.

Shambulizi limetokea wakati wa maombi ya adhuhuri, katika mji wa Mazar-e-Sharif, mkoa wa Balkh, ulio kaskazini mwa Afgnaistan.

Mkuu wa hospitali kubwa ya sehemu hiyo ya Abu Ali Sina-e-Balkhi, Ghousuddin, ameambia sauti ya Amerika kwamba watu sita kati ya waliojeruhiwa walikuwa katika hali mbaya.

Walioshuhudia tukio hilo amesema kwamba huenda idadi ya watu waliokufa ni kubwa kuliko ilivyotangazwa.

Kundi la wanamgambo la IS-Khorasan, lenye ushirikiano na kundi la Islamic State limedai kutekeleza shambulizi hilo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG