Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 18:24

Waasi nchini Syria washambulia kituo cha afya


Mwanamke wa Syria aliyejeruhiwa

Mashambulizi ya anga yameendela leo Ijumaa nchini Syria ambako kituo cha afya kilishambuliwa vikali katika mji wa Aleppo ambao ni pili ukubwa nchini humo.

Kituo hicho cha ambacho kilikuwa kikitoa matibabu kwa magonjwa sugu, pamoja na matibabu ya meno, kilishambuliwa siku moja baada ya hospitali kuharibiwa katika vurugu hizo, maafisa wa ulinzi wa kiraia walisema.

Muuguzi mmoja ni miongoni mwa waliojeruhiwa. Vyombo vya habari vya serikali vinaripoti kwamba waasi waliushambulia msikiti mmoja mjini Aleppo katika ujirani wa Bab al Faraj na kuuwa watu wasiopungua 15 na kuwajeruhi 30.

XS
SM
MD
LG