Shambulio la anga la Israel kwenye gari huko Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na Israel liliwaua Wapalestina watano, kwa mujibu wa jeshi la Israel na mamlaka ya afya ya Palestina, wakati ghasia zikiendelea katika eneo linalokaliwa na Israel.
Jeshi la Israel limesema vikosi vyake vilishambulia gari iliyokuwa imewabeba wanamgambo watano katika eneo la vijijini kaskazini magharibi mwa mji wa Tulkarem, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi mapema Jumamosi asubuhi, wakati wapiganaji hao walipokuwa njiani kutekeleza shambulio.
Wizara ya afya baadaye ilithibitisha kuwa watu watano waliuawa katika shambulio hilo na walipelekwa katika hospitali iliyo jirani ya Tulkarem. Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa shirika la Associated Press na mashahidi, mlipuko huo ulitokea katika barabara inayounganisha vijiji vya Palestina vya Zeita na Qaffin.
“Nilikuwa nakwenda kazini asubuhi, nilisikia mlipuko hapa karibu na nyumba,” alisema Taiser Abdullah, mkazi wa Zeita. Shirika rasmi la habari la Palestina, Wafa limesema miili minne ilichomwa moto na kuungua hadi kushindwa kutambuliwa” kutokana na mlipuko huo.
Forum