Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 12:29

Watano wapoteza maisha katika shambulizi la Mogadishu


Mwanajeshi wa kisomali akiwa kasimama karibu na jengo lililoharibiwa nje ya kituo cha polisi mjini Mogadishu Jumatatu Mei 9, 2016..
Mwanajeshi wa kisomali akiwa kasimama karibu na jengo lililoharibiwa nje ya kituo cha polisi mjini Mogadishu Jumatatu Mei 9, 2016..

Takriban watu watano wameuawa na wengine kumi na tatu kujeruhiwa baada ya mlipuko na milio ya bunduki katika makao makuu ya polisi wa trafiki, mashariki mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Hayo ni kulingana na ripoti za hospitali na Mashahidi. Wanamgambo wa Al-Shabaab wamedai kuhusika na mashambulizi hayo. Mashahidi walisema kwamba walisikia mlipuko mkubwa uliofuatiwa na mlio wa bunduki kwenye lango la makao makuu ya polisi wa barabarani karibu na bandari ya zamani, katika wilaya ya Shangani. Makao hayo makuu ya polisi wa barabarani yako karibu na ubalozi wa milki za kiarabu.

Bomu lililokuwa kwenye gari lililipuka, na muda mfupi baadaye, mwanamgambo mmoja alijaribu kuingia kwenye jengo hilo, lakini akapigwa risasi na polisi, Ripoti za Kiusalama zimeimbia Sauti ya Amerika.

XS
SM
MD
LG