Mpango wa Umoja wa Afrika huko Somalia (AMISOM) umeleeza kwamba umepata ripoti za mashambulizi kwenye kambi zake za kijeshi kwa majeshi ya Ethiopia na Somalia.
Kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab lilidai jaribio hilo la mashambulizi kwenye kambi ya jeshi ya Ethiopia limeuwa wanajeshi 60 wa AMISOM. Hata hivyo madai haya yamekataliwa na AMISOM na serikali ya Somalia.
Hili ni shambulizi la nne kwa ukubwa na kundi hilo la wanamgambo dhidi ya kambi za jeshi za Umoja wa Afrika huko Somalia katika mwaka.
Shambulizi hilo lilitokea asubuhi ya Juni 9 wakati ambapo wakazi walikuwa wakitoka kwenye sala za alfajiri wakati gari lililojaa milipuko liliposogezwa kwenye lango kuu la kambi ya kijeshi ya Ethiopia ambapo ililipuka.