Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 09:44

Waasi wa Taliban washambulia jengo la usalama mjini Kabul


Majeshi ya usalama ya Afghanistan yamesimama karibu na magari yaliyoharibiwa na mlipuko uliotokea mji mkuu Kabula april 19, 2016.
Majeshi ya usalama ya Afghanistan yamesimama karibu na magari yaliyoharibiwa na mlipuko uliotokea mji mkuu Kabula april 19, 2016.

Kundi la waasi wa Taliban limefanya shambulizi la kutumia bomu na bunduki mjini Kabul leo asubuhi, na kuwaua watu wasiopungua 30 na kuwajeruhi wengine 327.

shambulizi lililenga jengo, ambalo maafisa wanasema ni makazi ya kikosi maalum cha jeshi la usalama la Afghanistan ambalo linafanya kazi chini ya idara ya upelelezi ya nchi hiyo inayohusika na kuwalinda maafisa wa serikali.

Shambulizi hilo lilianza saa tatu asubuhi saa tatu asubuhi kwa saa huko, pale mlipuaji bomu wa kujitoa mhanga alipovurumisha gari yake iliyojaa milipuko kwenye eneo hilo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Sediq Siddiqi amewaambia waandishi wa habari, mamia ya kilo za milipuko ilikuwa imejazwa kwenye gari hiyo. Amesema wachunguzi wanaendelea na uchunguzi kufahamu idadi ya washambuliaji lakini amekiri kuwa kulikuwepo na mapungufu ya kiusalama na kupelekea shambulizi hilo ambalo limesababisha vifo.

XS
SM
MD
LG