Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 20:54

Idadi ya vifo katika shambulizi la Kabul yafikia 64


Mtendaji mkuu wa Afghanistan Abdullah Abdullah katikati akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo ambalo Taliban imedai kuhusika na shambulizi katika mji mkuu Kabul.

Maafisa wa Afghanistan wanasema idadi ya vifo kutokana na shambulizi la Taliban la kujitoa mhanga mjini Kabul imepanda kwa 64 na wengine 347 kujeruhiwa.

Idadi ya karibuni inaashiria kuwa shambulizi la Jumanne lilikuwa baya sana kufanywa na waasi katika mji mkuu wa Afghanistan tangu Taliban ilipoondolewa madarakani mwaka 2001.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Sediq Sediqqi amewaambia waandishi wa habari mjini Kabul Jumatano kuwa uchunguzi wa ngazi ya juu unaendelea kufahamu hali iliyopelekea shambulizi la mauaji katika eneo lenye ulinzi mkali sana.

Shambulizi hilo lililenga ofisi ya kurugenzi ya usalama wa taifa (NDS), idara ya upelelezi ya Afghanistan ambazo ziko katikati ya mji, si mbali kutoka makazi ya rais na ubalozi wa Marekani. Maafisa wamesema mapambano makali yamezuka kati ya washambuliaji na majeshi ya usalama ya Afghanistan ambayo yalidumu kwa saa kadhaa, na kusababisha washambuliaji wote kufariki, wengine wakijilipua wenyewe.

XS
SM
MD
LG