Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 09:59

Jeshi la Syria lashutumiwa kuishambulia kambi ya wakimbizi


Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa ameitisha uchunguzi dhidi ya mashambulizi ya anga kwenye kambi moja ya wakimbizi nchini Syria ambayo yameua dazeni ya watu jana Alhamisi, huku akisema shambulizi hilo huenda likawa ni uhalifu wa kivita.

Takriban watu 30 waliuawa katika kambi ya Kamuona, iliyo karibu na Sarmada, kaskazini mwa mkoa wa Idlib, huku dazeni za wengine wakijeruhiwa kwenye shambulizi hilo la kupitia angani. Hayo ni kwa mujibu wa kamati za mipango ambazo ziko kwenye mtandao wa wanaharakati wanao wanaompinga Rais Bashar Al Assad.

Kundi la wanaharakati la Syrian Observatory for Human Rights, lenye makao yake nchini Uingereza, limesema idadi ya waliokufa ni 28, wakiwa ni pamoja na watoto na wanawake. Hata hivyo, kundi hilo lilionya kwamba huendea idadi hiyo ikaongezeka.

XS
SM
MD
LG