Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 18:16

Shambulizi kaskazini mashariki mwa Kenya lauwa watu


Wanamgambo wa al-Shabab

Maafisa wa Kenya washuku kundi la al-Shabab kuhusika na shambulizi

Polisi katika mkoa wa Kaskazini Mashariki mwa Kenya wanasema shambulizi karibu na mpaka wake na Somalia limeuwa watu sita wakiwemo maafisa wanne wa polisi. Maafisa nchini humo wanasema watu waliokuwa na silaha walifyatua risasi pamoja na kifaa kilicholipuka kwenye kambi ya polisi katika mji wa Gerille jana jioni. Maafisa wa mkoa huo wanasema miongoni mwa waliouawa ni pamoja na afisa wa uhamiaji na raia mmoja. Walisema watu 13 hawajulikani waliko kufuatia shambulizi hilo. Hakuna kundi lililodai kuwajibika kwa shambulizi hilo lakini maafisa wa Kenya katika siku za nyuma wamelilaumu kundi la kiislam la wanamgambo wa al-Shabab kutoka Somalia. Majeshi ya Kenya yaliingia Somalia mwezi Oktoba kupigana dhidi ya al-Shabab , kundi ambalo Kenya inalaumu kwa utekaji nyara ndani ya ardhi yake na kwenye mpaka wake na Somalia. Na ripoti iliyotolewa Alhamis na kundi la kutetea haki za binadamu lenye makao yake New York inasema maafisa wa Kenya wanawapiga raia wenye asili ya Kisomali na kuwazuilia kwenye mpaka baina yake na Somalia wakiwemo raia katika mji wa Garissa ulioko Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG