Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:51

Shambulizi Kanisani Nigeria liliuwa watu 22


Afisa wa polisi akiwa katika ulinzi ndani ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Francis, siku moja baada ya shambulio lililowalenga waumini huko Owo, Nigeria, Jumatatu, Juni 6, 2022. (AP/Sunday Alamba).
Afisa wa polisi akiwa katika ulinzi ndani ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Francis, siku moja baada ya shambulio lililowalenga waumini huko Owo, Nigeria, Jumatatu, Juni 6, 2022. (AP/Sunday Alamba).

Shambulizi la Jumapili dhidi ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Francis katika mji wa Owo nchini Nigeria liliua watu 22 na kujeruhi 50, afisa wa Shirika la Kitaifa la Kudhibiti Dharura alisema Jumanne

Shambulizi la Jumapili dhidi ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Francis katika mji wa Owo nchini Nigeria liliua watu 22 na kujeruhi 50, afisa wa Shirika la Kitaifa la Kudhibiti Dharura alisema Jumanne.

Washambuliaji wasiojulikana waliwashambulia waumini kwa bunduki na vilipuzi wakati wa misa ya Jumapili ya Pentekoste. Mamlaka hazikuwa zimetoa takwimu zozote za majeruhi hapo awali. Ripoti za vyombo vya habari zilisema zaidi ya watu 50 waliuawa.

Ni jambo la kawaida kwa takwimu zinazokinzana za waathiriwa kujitokeza baada ya maafa nchini Nigeria.

Mamlaka haijatoa taarifa yoyote kuhusu utambulisho wa washambuliaji au nia yao.

XS
SM
MD
LG