Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 23:38

Shambulizi dhidi ya mkuu wa jeshi wa zamani Uganda


Shambulizi dhidi ya mkuu wa jeshi wa zamani Uganda
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:04 0:00

Hali ilivyokuwa baada ya mkuu wa jeshi wa zamani Uganda kujeruhiwa na mtoto wake wa kike kuuwawa baada ya watu wenye bunduki kulipiga risasi gari walilokuwa ndani yake mapema Jumanne iliyopita.

Jenerali Katumba Wamala, ambaye anatumikia wadhifa wa waziri wa kazi na usafirishaji katika serikali ya Uganda alijeruhiwa katika mkono wake huko nyumbani kwake nje ya mji wa Kampala, makao makuu ya Uganda, kulingana na msemaji wa jeshi Brigedia Flavia Byekwaso. Katika tukio hilo dereva wa Wamala na binti yake waliuawa.
Inaaminika watu waliowashambulia ambao hawajulikani walikuwa wanaendesha pikipiki ambazo zilikaribia gari ya waziri katika mtaa uliokuwa na harakati nyingi.
Walipiga bunduki sio chini ya mara saba, kwa mujibu wa kituo cha matangazo cha Uganda, NBS.
Video kutoka katika eneo la tukio linaonyesha waziri akiwa amelowa damu akiwataka wampeleke hospitali.


Facebook Forum

XS
SM
MD
LG