Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:01

Shakira akataa ‘ofa’ ya waendesha mashitaka kwenye kesi ya ushuru


ESPAÑA-SHAKIRA-IMPUESTOS
ESPAÑA-SHAKIRA-IMPUESTOS

Mwanamuziki  wa Colombia Shakira amechagua kwenda mahakamani badala ya kukubali makubaliano yaliyopendekezwa  na waendesha mashtaka wa Uhispania ili kutatua madai ya kuilaghai serikali ya nchi hiyo  ushuru wa dola milioni 15, timu yake ya uhusiano wa umma ilisema Jumatano.

Shakira, mwenye umri wa miaka 45, anaamini kuwa hana hatia na anachagua kuliaciha suala hilo mikononi mwa sheria, kampuni ya mahusiano ya umma ya Llorente y Cuenca (Yorente Kuenka) ilisema katika taarifa yake.

Waendesha mashtaka wa Uhispania walimshtaki mwimbaji huyo mwaka 2018 kwa kutolipa ushuru wa euro milioni 14.5 kwa mapato yaliyopatikana kati ya 2012 na 2014.

Anakabiliwa na uwezekano wa kutozwa faini na kifungo, iwapo atapatikana na hatia ya kukwepa kodi.

Hakuna maelezo ya haraka yaliyopatikana kutoka kwa waendesha mashtaka juu ya mpango huo. Hakuna tarehe ya kesi iliyopangwa.

XS
SM
MD
LG