Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:31

Shaba zilizoibiwa Nigeria zarejeshwa baada ya karne moja


Oba wa Ufalme wa Benin, Oba Ewuare II amepokea mabaki mawili ya sanaa yaliyoibiwa kutoka Uingereza.
Oba wa Ufalme wa Benin, Oba Ewuare II amepokea mabaki mawili ya sanaa yaliyoibiwa kutoka Uingereza.

Shaba mbili za mji wa Benin zilirejeshwa siku ya Jumamosi kwenye kasri ya kitamaduni nchini Nigeria,

Shaba mbili za mji wa Benin zilirejeshwa siku ya Jumamosi kwenye kasri ya kitamaduni nchini Nigeria, zaidi ya karne moja baada ya kuporwa na wanajeshi wa Uingereza, na hivyo kuibua matumaini kwamba maelfu zaidi ya vitu vya kale vinaweza kurejeshwa katika nyumba za mababu zao.

Vitu hivyo vya sanaa, vingi vikiwa huko Ulaya , viliibiwa na wavumbuzi na wakoloni kutoka Ufalme wa Benin uliokuwa mkubwa, ambako sasa ni kusini magharibi mwa Nigeria, na ni miongoni mwa vitu muhimu vya urithi wa Afrika. Vilitengenezwa mapema katika karne ya 16 na kuendelea, kulingana na Makumbusho ya Uingereza.

Katika hafla ya kupendeza ya kuashiria kurudi kwa sanamu ya jogoo na kichwa cha Oba au mfalme, msemaji Charles Edosonmwan wa jumba la Oba katika Jiji la Benin alibainisha kuwa baadhi ya shaba hizo zilihifadhiwa hadi New Zealand, Marekani na Japan.

Vifaa hivyo viwili vilikabidhiwa kwa Tume ya Juu ya Nigeria mwezi Oktoba na Chuo Kikuu cha Aberdeen na Chuo Kikuu cha Yesu huko katika chuo Kikuu cha Cambridge lakini bado havijarudishwa nyumbani kwa mababu zao. Sio sanaa tu bali ni vitu vinavyosisitiza umuhimu wa hali yetu ya kiroho," Edosonmwan alisema katika mahojiano pembeni mwa sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa kimila.

Kurudishwa kwa vifaa hivyo ni hatua nyingine muhimu katika mapambano ya miaka mingi ya nchi za Kiafrika kurejesha kazi zilizoporwa, kwani taasisi nyingi za Ulaya zinapambana na urithi wa utamaduni wa kikoloni.

XS
SM
MD
LG