Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 22, 2025 Local time: 09:03

Seneta Jeff Sessions anatarajiwa kupitishwa kuwa Mwanasheria Mkuu


 Seneta Jeff Sessions
Seneta Jeff Sessions

Warepublikan wana sauti kwenye baraza na wanahitaji kura chache za ziada ili kumpitisha mteule wa Rais Donald Trump.

Sessions amekabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Wademokrat ambao wanahoji rekodi yake juu ya uhamiaji na haki za wananchi, na tayari wamesema kuwa yuko karibu sana na Trump kuweza kufuata utawala wa sheria na kuliko kuleta siasa.

Warepublikan wamtetea Sessions

Hata hivyo Warepublikan wanamtetea Sessions, wakisema utendaji wake wa muda mrefu katika baraza la seneti umeonyesha wazi uadilifu wake.

Kura ya kumthibitisha imecheleweshwa katika harakati za Wademokrat kutumia kanuni za Baraza la Seneti kuvuta muda ili kuendelea kumzungumzia Sessions katika ukumbi huo.

Wakati wa mahojiano ya kuthibitishwa kwake mbele ya Kamati ya Sheria ya Seneti, Wademokrati walitumia kanuni ambayo haitumiki sana kuchelewesha kura kwa siku moja.

Wademokrat wamefanya hiana

Wabunge wa Warepublikan na Trump wamelalamika kuwa Wademokrat wanafanya hiana kuchelewesha mchakato wa kuthibitishwa kwa baraza la mawaziri la rais.

Wademokrat wamedai kuwa lazima wateule wachunguzwe kikamilifu, kwani baadhi yao wamechelewa kupeleka maelezo yao kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kimaadili.

Muendelezo wa majadiliano juu ya Sessions ulioanza Jumanne na kuendelea mpaka Jumatano ulifunikwa na Warepublikan kwa kumuonya Seneta wa Demokrat Elizabeth Warren.

Kauli ya Mjane wa Martin Luther King Jr

Alikuwa anasoma barua iliyoandikwa na Coretta Scott King, mjane wa kiongozi Martin Luther King Jr aliyeuawa katika harakati za kutetea haki za wananchi.

Barua ilitumwa kwa Kamati ya Sheria ya Seneti mwaka 1986 wakati Sessions alipotajwa kwa nafasi ya ujaji wa mahakama Kuu.

Kiongozi wa walio wengi katika Seneti Mitch McConnell amesema Warren alivunja kanuni za Baraza la Seneti kwa kumkataa Sessions, na amezuiliwa kuongea zaidi.

Seneta Warren Ajibu malalamiko ya McConnell

Warren alijibu hilo kwa kuweka kwenye Facebook picha ya video akiwa nje ya ukumbi wa Seneti uliokuwa unamuonyesha anasoma hiyo barua, ambapo King ameeleza “ upinzani wa nguvu” kwa Sessions kuwa ni jaji wa Alabama.

King amesema Sessions, wakati huo ni mwendesha mashtaka wa serikali kuu, alikuwa dhidi ya raia weusi kutumia haki yao ya kupiga kura, na alipata “motisha wa kisiasa kuendesha mashtaka ya uongo”na “kupuuza uvunjaji wa sheria wa haki za wananchi” mambo yanayoonyesha wazi kwamba hana sifa za kuweza kuwa jaji.

Sessions Ajitetea

Wakati wa mahojiano ya kuthibitishwa kwake, Sessions alijibu tuhuma hizo za ubaguzi kwa kusema kuwa zilikuwa “uongo uliozushwa.”

Video iliyoonyesha mahojiano hayo na Sessions iliangaliwa na watu milioni 3.8 na kusambazwa mara 91,000 katika saa nane za kwanza tangu kupostiwa.

XS
SM
MD
LG