Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:59

Serikali ya Zanzibar yazuia meli 5 kutoa huduma


Jahazi ya uvuvi ya Zanzibar ikisafirisha walonusuriuka na ajali ya Spice Islander
Jahazi ya uvuvi ya Zanzibar ikisafirisha walonusuriuka na ajali ya Spice Islander

Serikali ya Zanzibar imezizuia meli tano kuendesha shughuli zake za usafiri visiwani humo, kutokana na hitilafu za kiufundi.

Miongoni mwa meli zilizozuiliwa kuendesha shughuli zake ni MV Serengeti, Nura, Buraq One na Two pamoja na Mubarak. Licha ya meli hizi kuzuiwa Jumatatu, lakini zimekuwa zikifanya shughuli zake za usafiri wa majini hasa Pemba na Unguja kwa muda mrefu bila kuingiliwa na serikali.

Hatua hii inafuatia kutokea kwa ajali ya meli ya MV Spice Islander hivi karibuni visiwani humo na kuuwa zaidi ya watu 200 wakiwemo watoto wadogo. Baada ya ajali hiyo serikali ya Zanzibar imeunda tume maalumu kuchunguza chanzo cha ajali hiyo ambayo serikali imekuwa ikilaumiwa kwa uzembe.

Baadhi ya watu walionusurika katika ajali ya MV Spice Islander waliviambia vyombo kadhaa vya habari kuwa meli hiyo ilikuwa imejaa kupita kiasi na ilionekana kuwa na tatizo la kiufundi.

Katika kuboresha hali ya usafiri wa majini na kuhakikisha janga baya kama hili halitokei tena, Sauti ya Amerika imefanya mahojiano na mheshimiwa balozi Seif Ali Iddi, makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, ambaye anaanza kuelezea sababu zilizopelekea serikali kusitisha huduma za vyombo hivyo vya majini.

XS
SM
MD
LG