Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:12

Upinzani Myanmar waibua hoja dhidi ya upotoshaji wa vyombo habari vya kimataifa


Maaandamano kupinga utawala wa kijeshi wa Myanmar's 2021 nje ya ubalozi wa Myanmar Embassy, Tokyo, Japan
Maaandamano kupinga utawala wa kijeshi wa Myanmar's 2021 nje ya ubalozi wa Myanmar Embassy, Tokyo, Japan

Serikali ya upinzani ya  Umoja wa Kitaifa ya Myanmar hivi karibuni iliibua hoja kuwa vyombo vya habari vya kimataifa vimepotosha maelezo juu ya muundo wake.

Serikali ya upinzani ya Umoja wa Kitaifa ya Myanmar hivi karibuni iliibua hoja kuwa vyombo vya habari vya kimataifa vimepotosha maelezo juu ya muundo wake.

Msemaji wa ofisi ya rais wa NUG aliiambia Sauti ya Amerika (VOA) Jumatano katika taarifa yake kuwa NUG sio serikali iliyo uhamishoni kwa sababu idadi kubwa ya viongozi waandamizi, akiwemo kaimu rais, pamoja na waziri mkuu na wengi katika baraza la mawaziri, bado wanaishi na kufanya kazi nchini Myanmar.

Mashirika ya kimataifa ya habari, yakiwemo Washington Post, New York Times, BBC na Al Jazeera wameitaja NUG kama "serikali iliyo uhamishoni," "serikali kivuli," na "serikali sambamba iliyo uhamishoni."

Kundi la utetezi, Baraza Maalum la Ushauri kwa Myanmar, pia limepaza sauti juu ya msimamo wa NUG kwamba haiko uhamishoni. Mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo, Chris Sidoti, alisema katika video iliyobandikwa kwenye mtandao wa Twitter mapema mwezi Februari, "nataka kusisitiza kwamba NUG haiko uhamishoni. Watu wengi wa NUG wako Myanmar. NUG haifanyi kazi kwa kujificha."

Baadhi ya mashirika ya habari ya Myanmar, kama vile shirika la habari la Mizzima lenye uhusiano na Sauti ya Amerika idhaa ya Burma, wanaitaja NUG kuwa ni "serikali sambamba ya Myanmar iliyo uhamishoni," lakini jarida la kwenye mtandao, Irrawaddy, linaieleza NUG kama "serikali ya kiraia."

Mwisho—

VOA News

XS
SM
MD
LG