Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 17:16

Uganda yakanusha uvumi wa adhabu ya kifo dhidi ya raia wake China


Madawa ya kulevya
Madawa ya kulevya

Wizara ya Mambo ya Nje nchini Uganda imekanusha ripoti kuwa kuna mpango wa serikali ya China kutekeleza adhabu ya kifo kwa wananchi 23 wa Uganda kutokana na makosa ya kusafirisha madawa ya kulevya.

Kumekuwa na orodha ya majina ya watu 23 yanayo zungushwa katika mitandao ya kijamii yakidai kuwa serikali ya China inapanga kutekeleza adhabu ya kifo dhidi ya watu hao kutokana na makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.

Lakini, Wizara ya Mambo ya Nje Jumatatu katika tamko lake imesema: “Hii ni kuujulisha umma kuwa orodha inayosambazwa ni ile ya wananchi wa Uganda ambao walihukumiwa adhabu ya kifo miaka mingi iliopita na wakapewa msamaha wa miaka miwili na mahakama za Uchina, na baadae adhabu hiyo ilipunguzwa kufikia kifungo cha maisha na ikapunguzwa tena kufikia miaka kadhaa.”

Margaret A. Kafeero, kaimu Mkuu wa Diplomasia ya Umma ameongeza kusema kuwa katika tamko hilo: “Sisi hatuna uhuru wa kuzungumzia matatizo ya kila mtu iwe katika vyombo vya habari au katika sehemu za umma lakini napenda kusisitiza kuwa kinachofahamika ni kuwa serikali ya Uchina haijapanga kuua wafungwa wowote wa Uganda kwa wakati huu.”

Kwa mujibu wa afisa huyu, pande mbili za serikali hizi zinaendelea kufanya mazungumzo ya pamoja kwa kesi mbalimbali ambazo bado hazijashughulikiwa.

“Taarifa hiyo inayoenezwa kuhusu kutekelezwa kwa hukumu ya kifo kwa watu hao ni uongo na tunaomba kwa kuheshimiana na kwa sababu ya wasiwasi wa familia hizo, watu wanaoeneza uvumi huu waache kufanya hivyo na wawe na hisia juu ya wengine wakati wanapoamua kusambaza uzushi kama huu,” amesema afisa huyo.

XS
SM
MD
LG