Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 09, 2024 Local time: 22:39

Serikali ya Tanzania yathibitisha kifo cha raia wake aliyeuawa baada ya kukamatwa na Hamas


Gari la Shirika la Msalaba Mwekundu likiwa limewabeba mateka wa Israel wenye asili ya Russia Novemba 26,2023. Picha na Belal Al SABBAGH / AFPTV / AFP
Gari la Shirika la Msalaba Mwekundu likiwa limewabeba mateka wa Israel wenye asili ya Russia Novemba 26,2023. Picha na Belal Al SABBAGH / AFPTV / AFP

Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania siku ya Alhamisi imethibitisha kifo cha mmoja wa Watanzania ambaye “aliuawa mara baada ya kukamatwa na Hamas” wakati wa mashambulizi ya Oktoba 7, huko Kusini mwa Israel.

Siku ya Alhamisi Waziri wa Mambo ya Nje, Januari Makamba amesema mamlaka “imearifiwa na serikali ya Israel kuwa Joshua Mollel, mwanafunzi wa Kitanzania aliyekuwa akisoma nchini Israel, ambaye alipoteza mawasiliano tangu Oktoba 7, 2023…aliuawa mara baada ya kukamatwa na Hamas.”

Waziri Makamba alisema kupitia mtandao wa X kuwa mamlaka ya Tanzania inafanya mipango kwa familia ya Mollel, akiwemo baba yake, kwenda Israel na afisa wa serikali “kukutana na balozi wetu na maafisa wa Israel na kupata taarifa zaidi” kuhusiana na kifo chake.

Serikali ya Israel iliwataja wanafunzi wawili kutoka Tanzania waliokuwa wakisoma nchini Isreal -- Clemence Felix Mtenga mwenye umri wa miaka 22 na Joshua Loitu Mollel mwenye umri wa miaka 21.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania ilitangaza kifo cha Mtenga mwezi uliopita, bila ya kutoa maelezo kuhusu mauaji yake

Wanafunzi hao wawili ni miongoni mwa vijana wa Kitanzania wapatao 260 ambao walikwenda Israel kwa mafunzo ya kazi kwa vitendo katika kilimo cha kisasa chini ya mpango wa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG