Maafisa wa usalama wa Sudan wamezikamata nakala zote za gazeti binafsi wakati serikali ikiendelea na msako kwa vyombo vya habari.
Mhariri mkuu wa al Ahdath, Adil al Baz aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakuna maelezo yaliyotolewa wakati wanajeshi walipoziharibu nakala zote zilipotoka kwenye mashine ya kuchapisha.
Hii si mara ya kwanza kwa serikali ya Sudan imeingilia kati vyombo vya habari nchini humo, licha ya katiba inayodai uhuru wa vyombo vya habari.