Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 01:11

Serikali ya Nigeria inafanya mazungumzo na Boko Haram.


Rais wa Nigeria Nigeria Goodluck Jonathan akiwa kwenye eneo lililoshambuliwa kwa bomu.

Rais Goodluck Jonathan yupo kwenye shinikizo kali na inasemekana serikali imeanza mazungumzo ya kusitisha mapigano na kundi la Boko Haram.

Nigeria inasemekana imeanza mazungumzo ya kusitisha mapigano na kundi la Boko Haram , linaloshutumiwa kwa mamia ya vifo kutokana na mabomu na upigaji risasi katika miezi 18 iliyopita.

Vyanzo vya habari vya kisiasa na kidiplomasia wakiongea kwa sharti la kutotajwa wamesema wasuluhishi wanapeleka ujumbe kati ya serikali na viongozi wa kijeshi.

Ripoti kutoka Nigeria zinasema Boko Haram imetaka wanachama wake wote waliokamatwa kuachiwa kutoka jela kama sharti la kusitisha mapigano. Serikali inafikiria pendekezo hilo.

Rais Goodluck Jonathan yupo kwenye shinikizo kali kurudisha usalama Kaskazini , ambako Boko Haram wamefanya mashambulizi kadhaa mengi yakilenga Polisi, maafisa wa serikali na viongozi wengine wenye mamlaka.

XS
SM
MD
LG